Fresh Production

The home of Entertaiment and Internet business

Lyrics

 


AMA ZAKE AMA ZANGU


LEAD
Siku hizi sina raha, na mke wangu nyumbani, nirudipo kazini humkuta, kajiinamia,

CHORUS- Pole, ee bwana!

LEAD
Nauliza vipi mke wangu mbona umekasirika, hushindwa kunijibu, hubaki analia.

CHORUS
Masikini, analia.

LEAD
Nazidi kumbembeleza sanasana mke wangu, mwisho nae akaamuwa, kunielezea.

CHORUS
Aaaaa! akasema

LEAD
Eti anafahamu mambo yangu yote, nifanyayo nikiwa kazini,
eti nina wanawake wengi sana miye, hivyo basi anataka tutengane,
namfikiria ampae maneno mke wangu, nami sitokubali, namsaka mbea huyo,
namfikiria ampae maneno mke wangu, nami sitokubali, namsaka mbea huyo.

CHORUS
Ama zake ama zangu, ole wake akae akijuwa labda nisimtambue.

LEAD
Nimeelewa nia yake nikutaka kunigombanisha,
imekuwa sikai nikafurahi mimi na mke wangu.

CHORUS
Mtu huyo adui yangu, kanitafuta kwa siku nyingi naona amenipata.

TALK
CHOKOCHKO, FITINA, UNAFIKI NA UCHONGANISHI VIMEZIDI
LAKINI SASA ATAPIGWA MTU JINI!!!!.

MDO MAMA MDO- kolekole-,MDO MAMA MDO-kolekole.
WANA MIWANI- hao wademadema na njia zao,
WATANZANIA- hao wademadema na njia zao,
WADAR ES SALAAM- hao wademadema na njia zao,
WANA WATANGA- hao wademadema na njia zao,
ARUSHA NAO- hao wademadema na njia zao,
WANA WA MWANZA- hao wademadema na njia zao,
MAFIA PEMBA ZANZIBAR- hao wademadema na njia zao,
MAKAO MAKUU DODOMA- hao wademadema na njia zao.

MDO MAMA MDO- kolekole-,MDO MAMA MDO-kolekole.
WANA MIWANI- hao wademadema na njia zao,
WA NAIROBI NAO- hao wademadema na njia zao
WA KAMPALA NAO- hao wademadema na njia zao
KIGALI RUANDA- hao wademadema na njia zao
WA BUJIMBURA NAO!.

Top
Home

 

PENZI NI KIKOHOZI

Ama kweli penzi ni kikohozi, kulicha huliwezi.

CHORUS
Penzi ni kikohozi kulificha huliwezi x 4

LEAD
Mapenzi yangu kwa yule kijana, nikaamuwa kumfanyia mambo yote,
ili anielewe, huku mimi, mwenzie naumia,
jitihada zangu zote, zakumfinyia jicho na kumpiga ukope,
ni kama najisumbuwa, hataki, hata kuniangalia,
nimetuma baruwa ya kwanza, ya pili na ya tatu,
kimya moja kwa moja, majibu, hataki kunirudishia,
leo hii shoga yangu, siri yangu nakupasulia, chondechonde nishauri
ni njia gani, mi mwenzio nitayotumia.

CHORUS
Kaza moyo mueleze, waziwazi ujue moja,
wajuwa penzi ni kikohozi, kulificha huliwezi.

LEAD
Kumwambia naogopa, sura yangu naona haya,
sijui nifanye nini, ili ajue nampenda.

Akipita nashituka, akisema naumia
anapotabasamu, moyo wangu unanenda mbiyo.

Kumwambia naogopa, sura yangu naona haya,
sijui nifanye nini, ili ajue nampenda.

Akipita nashituka, akisema naumia,
anapocheka, meno yake, yanan'garan'gara.

RAP 1
Jamani kina dada, angalieni kina kaka wanagombania ngoma ngoma siyo yao yakucheza sindina sindimba!, EEH!, sindimba AAH!, Aaah! kumbe ni wewe!

Rap 2
We,we,we kijana, we kijana unafanya nini sasa tabia gani ya kutsa watu bila sababu eh!, eh!eh!, mwenzio anakupenda amekutumia baruwa chungu nzima hutaki kuzijibu kwanini? kwanini?, unadhani wewe ndiyo mrembo pekeyako katika dunia hii ya leo? wacha wako wengi sana!, mjibu mwenzio aelewe moja kama hutaki ajue kama unataka ajue kuliko kunyamaza!, kitendo kama hicho ukifanyiwa wewe utasikia vizuri? nauliza vizuri? utafurahi kweli? ah! acha maringo mpe jibu moja mwenzio!.

 

KIZABIZABINA

Kizabizabina mwana wa hali, kipi kikusikitishacho?.
yakupatayo leo ndiyo matunda ya juhudi zako,
kama juhudi hizo ungezitumia kwenye kazi, ungekuwa mtu wa maendeleo sana,
lakini leo kila upitapo watu wanakusema.


CHORUS
Kaja kaja miguu ya ufagio,kaja kaja miguu ya ufagio,
fanya uondoke utawaudhi wenzio.

LEAD
Unanisikitisha ndugu yangu we, kwa tabia uliyonayo ya ufagio,
kufagia lililo lako na lisilo la kwako,
umefanya watu wakupachike majina, wengine wanakuita kizabizabina,
na wengine wanakuita mdaku wa kudakuwa,

CHORUS
Kaja kaja miguu ya ufagio,kaja kaja miguu ya ufagio,
fanya uondoke utawaudhi wenzio.

LEAD
Umekuwa mtu wa kuhangaika huku na kule, kutafuta mambo ili uyachukue,
madogo hata makubwa kwako wewe ni sawa,
ukishayapata unaongeza chumvi na pilipili, na kuyapeleka kule sehemu ya pili,
watu wakigombana kwako wewe ni furaha.

CHORUS
Kaja kaja miguu ya ufagio,kaja kaja miguu ya ufagio,
fanya uondoke utawaudhi wenzio.

LEAD
Sasa jamaa wamekushitukia, wanakumulika kila unapozamia,
kila unapokwenda jamaa wamekupania,
hawana haja ya kukupiga wala kukuvamia, bali ni kukucheka na kukuachilia,
na unapotokea wao wanakukimbia.

CHORUS
Kaja kaja miguu ya ufagio,kaja kaja miguu ya ufagio,
fanya uondoke utawaudhi wenzio.

DAR ES SALAAM - hawakutaki,
MOROGORO - wamekuchoka,
TANGA - wamekususa umbea umekuzidi
UNGUJA NA PEMBA - wahawakutaki
MAFIA - wamekuchoka
NA MTWARA YOTE wamekususa umbea umekuzidi

LEAD
Sasa umegunduwa kuwa ulipofikia, ni pabaya,
unaanza kujifaragua, na kujikombakombakomba kwangu,
kujipitishapitisha na kujichekeshachekesha kwangu hakukusaidii,
kutaka urafiki na mimi ukidhani sijui mambo yako, hello, umekwama leo.

MWANANYAMALA - hawakutaki
KINONDONI - wamekuchoka
OYSTERBAY - wamekususa umbea umekuzidi
MAGOMENI - hawakutaki
MSASANI YOTE - wamekuchoka
PAKA UBUNGO - wamekususa umbea umekuzidi

LEAD
Kwahiyo ushauri wa pekee nitakaokupatia, mwana wa halali we,
ni kujaribu kurekebisha tabia yako na kuishi vema na watu wa mitaani,
badilisha tabia yako, badilisha mwenendo wako, badilisha mfumo wa maisha yako
na ukifanikiwa kubadilika, nasi tutakupokea.

NA ILALA - hawakutaki
KARIAKOO YOTE - wamekuchoka
MPAKA CHAN'GOMBE - wamekususa umbea umekuzidi
BUGURUNII - hawakutaki
VINGUNGUTI - wamekuchoka
MPAKA GONGO LA MBOTO - wamekususa umbea umekuzidi

LEAD
Hello, hello kizabizabina wewe,
utakuwa mgeni wa nani sasa uko kwenye matatizo, fikiria,
unaendekeza majungu, fitina na unafiki tu,
hivyo upende usipende, utake usitake, nakwambia acha, uzabizabina.

MAKORORA - hawakutaki
USAGARA YOTE - wamekuchoka
NGAMIANI - wamekususa umbea umekuzidi
MSAMBWENI - hawakutaki
NA MAJENGO YOTE - wamekuchoka
MAPINDUZI - wamekususa umbea umekuzidi
BUYUNI KITOPENI - hawakutaki
BAGAMOYO - wamekuchoka
MPAKA PANGANI - wamekususa umbea umekuzidi
MOSHI NA ARUSHA - hawakutaki
DODOMA NA MWANZA - wamekuchoka
HATA SHINYANGA - wamekususa umbea umekuzidi
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
CHORUS
Hello, hello, kizabizabina umekwama leo mama.

LEAD
Umekwama sababu ya tabia yako,
Mmmmmmmmmm!!!!!!!!  mh!. wacha!

CHORUS
Hello, hello, kizabizabina umekwama leo mama.

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Guitar
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
CHORUS
Hello, hello, kizabizabina umekwama leo mama.

LEAD
Angalia jamii inakutenga leo,
utamlilia nani huna rafiki,
walikuonya kuhusu tabia yako,
mmmmmmmmmmmmm!!!!!!!!!!!!
ukajiona wewe ni operator
kuwaunganisha watu kwa mabaya
ukajifanya wewe ni speaker
kuyasema yasiyokuhusu
kujifanya wewe ni mpelelezi
kuchunguza yasiyokuhusu 

MWANAMBUZI

Kinyuli nyulika, mwanangwa wa Jumbe, kavaa nguo mbili,
yatatu kajifunika, aliye juu aondoe.

MWANAMBUZI MEE! MEE! - kamlilia mwanawe
KAMWAMBIA KWERA - kwera mlima una mawe

 


NAIMA

Naamini, ulizaliwa ili uwe na mimi Naima, Naima.
Naamini, nilizaliwa ili niwe na wewe Naima, Naima wa roho.

Wakati mwingine, nakuchukia sana sana Naima,
na ninapokuchukia Naima ni sababu nakupenda sana Naima, Naima wa moyo.

Unaponiudhi Naima, nachukulia hiyo ni bahati mbaya tu,
lakini nikikuudhi Naima, lazima nitubu nimefanya kosa nastahili kuadhiniwa Naima
Naima, Naima

Naima, Naima, Naima, Naima Naima!.
Ninapokuwa na wewe Naima, najihisi napasuwa raha, katikati ya shida Naima,
Roho yangu, nakuachia wewe mpenzi Naima,
Akili yangu, nakuachia wewe mpenzi Naima,
Mwili wangu nakuachia wewe mpenzi Naima,
Mahela yangu yote, nakuacha wewe mpenzi Naima,
Maisha yangu, yako mikononi mwako darling Naima, Naima.

Sura yako, inaniumiza mpenzi Naima, umbile lako, linaniumiza mpenzi Naima.

 

FUNGUWA MACHO

Amka, simama tembea utafute bahati yako,
funguwa macho, angalia mbele usilalie masikio, utakufa masikini kijana ah!,
wakale walisema mama, muomba mungu hachoki,
na anapochoka, huwa amekwishapata,
ukikaa chini ukinyanyua mikono juu, kumuomba mungu baba, oh! baba
ukidhania utapata ndugu wangu wewe hapo utakuwa

UNAJIDANGANYA TU -  Hapo utakuwa wewe
UNAJIDANGANYA KAKA - Amka ufanye kazi
UNAJIDANGANYA TU - acha kuombaomba
UNAJIDANGANYA KAKA.
MUNGU MWENYEWE ANASEMA JISAIDIE NIKUSAIDIE
HAPANA KUOMBA

Usilalie masiko, funguwa macho.

DUNIA YA LEO
USILAZE DAMU
AMKA MAPEMA
KATAFUTE KAZI
UKILALA SANA
UTAPITWA NA MAMBO
KABLA HUJAFA
USIKATE TAMAA
ACHA KUZUBAA
FANYA BIDII.

Ye,ye,ye, kijana unalala sana unategema nani, akusaidie katia maisha yako wewe mwenyewe. Amka, simama, toka ukajaribu kutafuta bahati yako, bahati haiji kitandani bali iko sehemu fulani, yakungoja, uifuate, uifuate. Hakuna lisilowezekana hapa duniani ni bidii yako tu nibidii yako tu anza sasa.

Fanya bidii, fanya kazi.

FANYA BIDII,  BIDII YA KAZI
UVIVU NA UZEMBE, HAVINA NAFASI
KUOMBAOMBA, KUMEPITWA NA WATI
POLE POLE POLE POLE, NDIYO MWENDO.

Usilalie masiko, funguwa macho.

DUNIA YA LEO
USILAZE DAMU
AMKA MAPEMA
KATAFUTE KAZI
UKILALA SANA
UTAPITWA NA MAMBO
KABLA HUJAFA
USIKATE TAMAA
ACHA KUZUBAA
FANYA BIDII.


 


DEMOKRASIA YA MAPENZI

Mama watoto, kaa chini nikuelezee demokrasia ya mapenzi, mmmmmmm!
mapenzi ni kupendana myoyoni kuingizana imani kuaminiana,
machoni kuangaliana midomokubusiana, wawili kukumbatiana,

shida kusaidiana ukweli kuambiana, maraha kupeana, hiyo ndiyo demokrasia,
demokrasia, ya mapenzi.

Sera zako nilizikubali, na sera zangu ukazikubali, na leo hii tumechaguana
tuongoze mapenzi yetu.  NIPE NIKUPE.

Mpenzi leo naahidi, niko hapa kwa ajili yako,
naketi mbele yako mama, fanya lolote utakalo.

Ninaishi kwa ajili yako, ninapumua kwa ajili yako,
nafanya kazi kwa ajili yako, niko tayari kuwa mtumishi wako mama,

Popote uendapo lolote ufanyalo nitakuwa nyuma yako mama,
nataka ufaidi matunda, matunda ya demokrasia ya mapenzi.

Na kwa yote hayo nataka na wewe unipe uhuru,
uhuru wa kusema, uhuru wa kufanya, na kuamuwa kuhusu mapenzi yetu.

Demokrasia, demokrasia, demokrasia,
Demokrasia, demokrasia, demokrasia ya mapenzi.

Ulitakalo kwangu, uniombe nami nitakupatia,
nilitakalo kwako, nitakuomba, tafadhali nawe unipatie, maah!,

Sema ukipendacho sema ukitakacho, nambie,
unipe nikinywacho unipe nikilacho, hiyo ndiyo demokrasia

Demokrasia, demokrasia, demokrasia,
Demokrasia, demokrasia, demokrasia ya mapenzi. 


MTI MKAVU

Nipande mti mkavu mbichi walewalewa,
kuna mahaba ya njiwa mke kumlisha mumewe,
wanawake wana magamba, wanaume wana sagamba,
iya magamba iya sagamba.

MAMAE! - JAMA Barazani kwangu -  MAMAE!
niupande mti gani - MAMAE!
Jama nikiupanda mpera - MAMAE!
Wahuni watanikera - MAMAE!
Jama nikiupanda mchungwa - MAMAE!
Unahitaji kuchungwa jama - MAMAE!
Jama nikiupanda mnazi - MAMAE!
Walevi wataniudhi - MAMAE!
Jama nikilifunga bembea - MAMAE!
nakaribisha umbea kwangu - MAMAE!
Jama barazani kwangu - MAMAE!
niupande mti gani jama - MAMAE
ALUME!, UCHI NA ACHE!

Chekelea,chekelea maisha ni limoja, hayarudi hayo!

HAYARUDI HAYO, YAMEPITA HAYO,
UKIPATA KITUMIE, UKIKOSA KIJUTIE MAMA.

Mla ni mla wa leo mla jana kala nini.

UTAMU WA UBWABWA WA LEO, TUNAUPATA LEOLEO,

Huu ni wakati wangu wangu wakati wako umepita

WAHATI WA MIMI, KUWASHA MOTO MAMA,

Mla ni mla wa leo mla jana kala nini.

KAMA ULIKULA CHAPATI LEO NI MAPOCHOPOCHO,

Huu ni wakati wangu wangu wakati wako umepita.

NAPASUWA RAHA KATIKATI YA SHIDA.

Chekelea,chekelea maisha ni limoja, hayarudi hayo!

HAYARUDI HAYO, YAMEPITA HAYO,

Chekelea,chekelea maisha ni limoja, hayarudi hayo!

KUMBE NI WEWE? AH!

Chekelea,chekelea maisha ni limoja, hayarudi hayo!

BOB CHIPEMBELE SAIDI CHIPEMBELE.

Chekelea,chekelea maisha ni limoja, hayarudi hayo!

AH, SAMUEL KUCHAKA, KUMBE NI WEWE

Mla ni mla wa leo mla jana kala nini.

MLA JANA KALA NINI, AMEPITWA NA WAKATI.

Huu ni wakati wangu wangu wakati wako umepita.

 

WAALIMU

A, E, I, O, U.

Tuwape heshima na unyenyekevu waalimu - WALIMU WETU WA CHEKECHEA.
Tuwape heshima na unyenyekevu waalimu - WALIMU WETU WA MSINGI
Kwani wao ndio mwanga wa maisha ya dunia - SEKONDARI NAO, NA VYUO VYOTE JAMANI - Kwani wao ndio mwanga wa maisha ya dunia.

Mmm,mmm,mmmh!,
Ayaiyaiyo, nakumbuka, miaka mingi leo imepita,
wazazi wangu wananishika mkono, kiguu na njia kuelekea shuleni
nakutana na waalimu wananipokea, sijui mbele oh!, sijui njuma mimi!
sijui moja, sijui mbili oh!, nakutana mwalimu mwalimu Halima,
ananipokea nakufanya mambo yake, sasa najuwa mambo yote,
mwanga wa maisha unaniongoza, kusoma najuwa kuandika najuwa,
mshahara wa kutosha napata oh!,
Walimu wetu we, tuwape heshima, walimu wetu we, tuwaheshumu jama oh!.

Tuwape heshima na unyenyekevu waalimu - TUWAPE MSHAHARA WAKUTOSHA
Tuwape heshima na unyenyekevu waalimu - MSHAHARA WAPATE MAPEMA
Kwani wao ndio mwanga wa maisha ya dunia - MARUPURUPU YAONGEZEKE WAFAIDIKE
Kwani wao ndio mwanga wa maisha ya dunia - WALIMU WETU WE!, WALIMU WETU WE OH!.

TUWAPE HESHIMA, WALIMU WA CHEKECHEA JAMA -
aa waalimu wetu eh!, waalimu
TUWAPE HESHIMA WAALIMU WA MSINGI JAMA
aa waalimu wetu eh!, waalimu
TUWAPE HESHIMA WAALIMU WA VIDUDU JAMA
aa waalimu wetu eh!, waalimu
TUWAPE HESHIMA WAALIMU WA SECONDARY JAMA
aa waalimu wetu eh!, waalimu
TUWAPE HESHIMA WAALIMU WA COLLAGE ZOTE
aa waalimu wetu eh!, waalimu
TUWAPE HESHIMA WAALIMU WA VYUO VIKUU JAMA
aa waalimu wetu eh!, waalimu
TUWAPE HESHIMA WAALIMU WOTE JAMA
aa waalimu wetu eh!, waalimu

Waalimu wetu tuwaheshimu,
WAPI MWALIMU HALIMA
Waalimu wetu tuwaheshimu
WAPI MWALIMU MUHINA WEWE
Waalimu wetu tuwaheshimu
WAPI MWALIMU MUSSAJI
Waalimu wetu tuwaheshimu
SHULE YA MAKORORA
Waalimu wetu tuwaheshimu
WALIMU TUSIWAPE TAABU
Waalimu wetu tuwaheshimu
TUWALIPE MSHAHARA WAO
Waalimu wetu tuwaheshimu
WAKATI UNAOSTAHILI
Waalimu wetu tuwaheshimu.

 


MALAIKA

Malaika wangu wewe, ni wewe, wakuilinda na kuitunza roho yangu isibabaishwe
isipitiwe na upepo mbaya.
Malaika wanguwe, jaribu kunichukuwa, uniweke ndani ya moyo wako,
wanitafute wasinione kabisa,
Kwani wabaya, hapa duniani, ni wengi sana, vizabizabina, wambea ni wengi
wanatuchimba, pangu pakavu, nitilie mchuzi, wanahangaika, wachawi ni wengi,
wanga ni wengi, tujiangalie,
MALAIKA - Nipokee mama,
MALAIKA WANGU WE - Ninakuja
MALAIKA - Nipokee,
MAIKA WANGU WE - Ninakuja.

Ubaya umemrudia - Umemrudia, umemrudia sasa anababaika.

Chelea chekelea chekelea kaka - Chekelea maisha ni limoja tu,
Furahia furahia furahia wewe - Chekelea maisha ni limoja tu.

 


MASKUZI

Nashangazwa, kwa malalamiko yako mzee Maskuzi,
unadai wanao hawakutunzi, jambo ambalo ulilisababisha wewe mwenyewe,
mzee mwenzangu.

Wakati unapewa urithi, nilikuwa shahidi wa pili, na wakwanza ni mzee Jumbe,
mbele ya wanao - ZANANA NAE ALIKUWEPO, NILISHUHUDIA.

Baba yako akakuambia, mwanangu Maskuzi, itunze minazi mia tatu hiyo,
ikusaidie wewe, pamoja na wajukuu zangu - JUMAA, MAEMBE NA RAMADHANI

Minazi umegema pombe, baadae umeiuza
ah! lawama zanini,
Minazi umegema pombe, baadae umeiuza
ah! lawama zanini wanao hawana kosa

Ingawa wana wajibu wa kukutunza baba yao, tabia ya kufilisi urithi mzee mwengu,
bila kujali kizazi chako ni mbaya sana, bila kujali kizazi chako ni mbaya sana.

Minazi umegema pombe, baadae umeiuza
ah! lawama zanini
Minazi umegema pombe, baadae umeiuza
ah! lawama zanini wanao hawana kosa

Jumaa ameoa, ana familia anaitafutia,
Maembe na yeye anajitahidi kadiri awezavyo,
Masikini Ramadhani, alijitahidi katika kutafuta,
Acha lawama zako, kwa wanao, wenyewe wana matatizo yao.

Minazi umegema pombe, baadae umeiuza
ah! lawama zanini
Minazi umegema pombe, baadae umeiuza
ah! lawama zanini wanao hawana kosa

Lakini nitawashauri wanao wasikutupe mkono,
kwa sababu eti uliuharibu urithi,
lazima wakumbuke kuwa wewe ni baba yao mzazi.

Minazi umegema pombe, baadae umeiuza
ah! lawama zanini
Minazi umegema pombe, baadae umeiuza
ah! lawama zanini wanao hawana kosa

NYU, NYU - NYUKWA!.

ETATEH!, IYOH, MASKUZI, ETATEH!
Acha lawama kwa wanao kaka
ETATEH!, IYOH, MASKUZI, ETATEH!
Wanao hawana kitu unawashambulia
ETATEH!, IYOH, MASKUZI, ETATEH!
Acha lawama kwa wanao kaka
ETATEH!, IYOH, MASKUZI, ETATEH!
Wenyewe wana familia zinawategemea
ETATEH!, IYOH, MASKUZI, ETATEH!
Mmmmmmmmmmmmmh!
ETATEH!, IYOH, MASKUZI, ETATEH!
Dunia ya leo imekuwa ngumu
ETATEH!, IYOH, MASKUZI, ETATEH!
Kila mtu anapaswa kujitegemea
ETATEH!, IYOH, MASKUZI, ETATEH!
Rrrr yah! - YAH!, Rrrr yah! - YAH!,
Kina baba mmechoka? - BADO!
Kina mama mmechoka? - BADO!

 


KABWELA

AMA KWELI RAFIKI NI MKIA WA FISI, USIPOANGALIA ATAKUFILISI.

Rafiki mwema utamjuwa wakati wa shida,
Mpenzi wa kweli utamtambuwa kwenye matatizo

OH! TUTAKUWA PAMOJA MPAKA MWISHO, SASA, KIKOWAPI?

Tulikuwa pamoja tukihangaikia maisha, Dar es salaam,
Tukaenda na yeye kutafuta maisha, mpaka Zanzibar,
Nikapata tatizo kidogo, mwenzangu, akaamuwa kunikimbia,
akaanza kupita mitaani na kusema, sina lolote
hakuna kitu nitapata nahangaika bure.

Rafiki mwema utamjuwa wakati wa shida,
Mpenzi wa kweli utamtambuwa kwenye matatizo

Tulikuwa na yeye tukihangaikia maisha, Zanzibar,
Tukaende na yeye kuchuma karafuu chakechake Pemba,
Nikapata tatizo kidogo, mwenzangu, akaamuwa kunikimbia,
akaanza kupita mitaani na kusema, sina lolote
hakuna kitu nitapata nahangaika bure.

Ah! nasikitika ulivyonifanyia, tena umenihuzunisha we Kabwela,
na urafiki wetu mimi nawe umekwishakufa.

Unakuja nyumbani kwangu na kuniomba nikusaidie,
sasa nitakusaidiaje na ulisema sina lolote.
Unakuja kwa magoti na kuniomba msamaha,
nitakusamehe vipi nawe ulitaka nisifanikiwe.

Ah! nasikitika ulivyonifanyia, tena umenihuzunisha we Kabwela,
na urafiki wetu mimi nawe umekwishakufa.

Unakuja nyumbani kwangu na kuniomba nikusaidie,
sasa nitakusaidiaje na ulisema sina lolote.
Unakuja kwa magoti na kuniomba msamaha,
nitakusamehe vipi nawe ulitaka nisifanikiwe.

Ah! nasikitika ulivyonifanyia, tena umenihuzunisha we Kabwela,
na urafiki wetu mimi nawe umekwishakufa.

Sikusema mbya we, uliyesema mbaya ni wewe
sikusema mbaya we, uliyesema mbaya ni wewe
ayayah! ayayah! uliyesema mbaya ni wewe,
ayayah! ayayah! uliyesema mbaya ni wewe.

Rafiki mwema utamjuwa wakati wa shida
ATAKUSAIDIA WAKATI WA SHIDA
Mpenzi wa kweli utamtambuwa kwenye matatizo
ATAKUWA NA WEWE BEGA KWA BEGA
Rafiki mwema utamjuwa wakati wa shida
ATAKUPA MAWAZO UNAPOYAHITAJI
Mpenzi wa kweli utamtambuwa kwenye matatizo
ATAKULIWAZA KWENYE UGONJWA
Rafiki mwema utamjuwa wakati wa shida
ATAKUPA USHAURI UNAPOUHITAJI
Mpenzi wa kweli utamtambuwa kwenye matatizo
HAWEZI KUKUCHEKA UNAPOKWAMA

 


NI VITA MTINDO MMOJA!

CHORUS-
Mapambano yameanza,
nahatujui yatakwisha lini, mapambano.
Mapambano hayo,
hatutashinda kama hatukushirikiana, wote.

LEAD-
Vita kubwa tuliyonayo,
nikupambana na maradhi ya ukimwi,
 Na silaha zetu tulizonazo,
ni uaminifu na kuelewa kwa makini,
Ni vipi tutajikinga,
na ugonjwa huu maana haujapata dawa,
Na vipi tutawaelimisha,
watoto wetu wasipatwe na balaa hilo,
Vita hii ni kubwa, tunapaswa kushirikiana,
kwa kushauriana,tubadilishe tabia zetu,
katika jamii yetu, kama tunataka kuishinda vita hii.

CHORUS-
Tusiwanyanyase, waathirika,
kwani wao hawakuomba, ni bora tuwe nao,
Tuzisaidie, familia zao,
kwani wao hawana nguvu tena za kuwatunza.

RAP-  
Kwa taarifa kamili tulizozipata,
toka kwa wataalam waliosifika,
Asilimia sabini duniani ya walioupata,
au kuathirika ni watu wa Africa,
Ni wajibu wetu sasa kuingia kwenye vita,
si vya mabomu bunduki wala ndege za vita
Bali kuhakikisha tabia njema tunazifuata,
na kufuata ushauri nasaha tunaoupata.

CHORUS-
Mapambano yameanza,
nahatujui yatakwisha lini, mapambano.
Mapambano hayo,
hatutashinda kama hatukushirikiana, wote.

LEAD- 
Kunusurika si ujanja, na kuathirika si ujinga,
muhimu ni kuwapa upendo,
wale waathirika ili kuwapa faraja,
na kutoa mafunzo zaidi,
kwa wanusurika ili kuinusuru jamii,
na tujilinde wenyewe,
tukilinde kizazi kipya, na pia tukilinde kizazi kijacho.

RAP-  
Mliokwisha athirika muangalie vizuri,
msije mkawapaka wasiokuwa na habari,
Kama mtu akikutaka muelezee dhahiri,
kwamba mimi nisingetaka kukuonjesha shubiri.

CHORUS-
Tusiwanyanyase, waathirika,
kwani wao hawakuomba, ni bora tuwe nao,
Tuzisaidie, familia zao,
kwani wao hawana nguvu tena za kuwatunza.

CHORUS-
Mapambano yameanza,
nahatujui yatakwisha lini, mapambano.
Mapambano hayo,
hatutashinda kama hatukushirikiana, wote.


 

BILA YA WEWE

Hey Miyoko, are you alright?,
listen, I wanna tell you something,
you know what?, I wrote this song special for you baby,
I mean really special for you, 
you know what I'm saying, hahah!.

LEAD(English)
You, you are the one I've been looking for,
you, you are the one I'll be taking care forever,
forever, forever I will love you,
where ever you are, what ever you do,
baby, I will be with you.

CHORUS(Japanese/Swahili)
Miyoko, kite, kite kudasai yoo
Miyoko, kite, kite kudasai yoo, karibu yangu.

LEAD(Swahili)
Nilipokuona mara ya kwanza, nilidhania ni malaika,
kanishukia mbele yangu, toka mbinguni, kwa Mungu,
sura uliyonayo na mwili wako si vya kawaida,
sogea karibu yangu unipe nafasi yangu, honey, iiiii.

CHORUS(Swahili)
Bila ya wewe, maisha si maisha tena,
bila ya wewe, sina nguvu ya kufanya kazi,
bila ya wewe, chakula hakina tamu tena,
bila ya wewe, usingizi siupati tena.

RAP(Swahili)
Nataka kukueleza yaliyomo moyoni mwangu baby, aah!,
maisha kamwe nisingeyaweza bila ya wewe kuwa wangu,
umenipata?,ndiyo maana ulipojitokeza
na kuingia kwenye anga zangu, mh!, nikakuona,
nikaamuwa kujipendekeza
na kukutia mikononi mwangu, baby
leo niko nawe, leo hii kwa upande wangu
naona pepo nimeipata,
kwa wewe kuwa mpenzi wangu roho yangu imetakata,
hebu sogea karibu yangu ili niwe nimekupakata,
na maneno yale ya walimwengu tuyakatae katakata.

CHORUS(Swahili/Japanese)
Miyoko, kite, kite kudasai yoo,
Miyoko, kite, kite kudasai yoo, karibu yangu.

LEAD(English)
You, you are the one I've been looking for,
you, you are the one I'll be taking care forever,
forever, forever I will love you,
where ever you are, what ever you do,
baby I will be with you.

CHORUS(Japanese/Swahili)
Miyoko, kite, kite kudasai yoo
Miyoko, kite, kite kudasai yoo, karibu yangu.

LEAD(Swahili)
Nilipokuona mara ya kwanza, nilidhania ni malaika,
kanishukia mbele yangu, toka mbinguni, kwa Mungu,
sura uliyonayo na mwili wako si vya kawaida,
sogea karibu yangu unipe nafasi yangu, honey, iiiii.

CHORUS(Swahili/RAP Japanese)
Bila ya wewe ANATA INAE TO,
maisha si maisha tena ORE NO JINSE DAME KAMO
bila ya wewe ANATA INAE TO,
sina nguvu ya kufanya kazi SHIGOTO MO DEKINAE SHI!
bila ya wewe ANATA INAE TO,
chakula hakina tamu tena TABEMONO MO OISHII KUNAE SHI!
bila ya wewe ANATA INAE TO,
usingizi siupati tena MO NEMURENAE YO!

RAP(Japanese)
Ne ne ne, wakatta kana? hah?
ja sukiyatte kudasai
kikoeru?, anone!  hahah, mmh! 
sukiyatte kudasai
onegaishimasu, onegai anone mh!
sukiyatte kudasai
I love you mh! hahaha!  ja!,  yoroshiku neh!.

 

SUGAR MUMMY

LEAD
Unajuwa wanadhania ninakupenda sababu ya pesa zako,
pia wanashangaa, umri wangu, na wako haulingani,
wanasema itakuwaje kijana kama mimi
kuwa na mama kama wewe,
wanasahau kuwa mapenzi hayajui mapesa
wala umri, wacha niwaambie leo.

CHORUS
Sugar mummy, amenipenda, nimempenda hatutaachana,
shida zake, ni shida zangu, raha zangu ni raha zake,
ayayayaya.

LEAD
Hatujali tofauti ya umri wetu,
tukiwa pamoja tunasahau utajiri wake
na umasikini wangu, tunajali mapenzi.

LEAD
She is the queen of hart, living in the house of cards. 

CHORUS
uuuu!, uuuu!, uuuu!, uu!, ayayayayaaaa!

LEAD
Hawajui mimi na wewe ni wapi tulipoanzia,
tulivuka mabonde milima na taabu tukiwa pamoja,
leo hii tunapasuwa raha kwao wao inawakera
acha niwaambie leo.

CHORUS
Sugar mummy, amenipenda, nimempenda hatutaachana,
shida zake, ni shida zangu, raha zangu ni raha zake,
ayayayaya.

LEAD
Tafadhalini tuacheni kama tulivyo,
pilipili iliyo shambani sijui nyinyi
inawawasha vipi, acheni maneno.

CHORUS
Uuuuuuya!, uuuuuuya!,
yaiyaiyaiyaiyaiyaah!.

LEAD
Unajuwa wanadhania ninakupenda sababu ya pesa zako,
pia wanashangaa, umri wangu, na wako haulingani,
wanasema itakuwaje kijana kama mimi
kuwa na mama kama wewe,
wanasahau mapenzi hayajui mapesa
wala umri wacha niwaambie leo.

CHORUS
Sugar mummy, amenipenda, nimempenda hatutaachana,
shida zake, ni shida zangu, raha zangu ni raha zake,
ayayaya.

LEAD
Tafadhalini tuwacheni kama tulivyo, pilipili iliyo shambani
sijui wenzangu inawawasha vipi acheni maneno.

 

AMINA

CHORUS-
Jambo, limezuwa mambo,
Amina, kweli umeumbika mamax2

LEAD-
Aa, lolololololo, jamani nimepatikana,
kweli nimepatikana, mwenzenu nimenasa miye,
macho yangu hayaoni tena,masikio hayasikii
mwili unaninyon'gonyea, na akili imedumaa,
kunajambo limenizukia miye.

CHORUS-
Jambo, limezuwa mambo,
Amina, kweli umeumbika mama

LEAD-
Nimeshawahi kuona, wazuri walioumbika,
wenye sura za kuvutia, na viuno vya kukata,
wenye matako ya kumimina, na miguu ya kumwaga,
lakini alivyo Amina, ni tofauti na yote hayo,
Amina, aliumbwa akaumbika,
anaponiangalia, mimi ninababaika,
macho ya kurembuwa, midomo ya kunyonya,
sijakamilika miye,bila ya kuwa na yeye, Amina.

CHORUS-
Jambo, limezuwa mambo,
Amina, kweli umeumbika mamax2

LEAD-
Amina, Amina,
makaratasi ya nyumba yangu, nakukabidhi Amina
funguo ya gari langu, nakukabidhi Amina,
nataka uwe wangu Amina, nami pia niwe wako,
nikutunze ipasavyo Amina, vile inavyostahili,
nikupeleke dukani, uchague nguo utakayo,
nikupeleke salon, uchague mtindo utakao,
nataka kuwajibika, nikutunze ipasavyo Amina,
nitimize mambo.

CHORUS-
Jambo, limezuwa mambo,
Amina, kweli umeumbika mama...............