Habari ndugu yangu. Pole na kazi. Pride FM inapenda sana kukufanyia interview huko kwa kutumia Skype. Pia unaweza sikiliza Pride FM online.
http://208.43.81.168:8874/stream?.wma Kipindi cha Afro Pride kuanzia saa kumi na mbili na nusu mpaka saa tatu usiku kinapiga sana mimbo yako.
Tunashukuru sana kwa jingles zako ambazo ulituandalia. Tafadhali naomba tukuinterview.
Kila la heri na kazi njema
Yes Fresh, unatisha kwa kazi zako ila nakumbuka wakati tunafanya kipindi cha Redio hapo Redio Tumaini ulisema kwamba utakuwa unarejea nchini mara kwa mara Je lini utarejea tena?
Nadhani unanikumbuka bradha. Mimi ni mwandishi wa habari wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo. Wakati wewe ulipokuwa uking'ara kimuziki, nilikuwa mwandishi wa gazeti la Mfanyakazi. Kwa kushirikiana na bosi wake, Hemed Kimwanga wakati ule, nakumbuka niliandika makala nyingio juu yako, ikiwemo ile baada ya wewe kurudi kwa mara ya kwanza nchini ukitokea Japan. Ulinisimulia habari nyingi za safari yako kimuziki, kuanzia ulipokwenda Kenya ukiwa na mpiga drums Chipembele Saidi, rafiki yako huyo alivyoshindwa maisha na kuamua kurejea Bongo na jinsi wewe ulivyobahatika kwenda Japan. Nakutakia kila la heri bradha katika maisha yako kimuziki.
Hi Brother Fresh,sisi ndio wadau wa muziki wako.Machachache nayoweza kusema ni kuwa miziki yako ipo katika kiwango cha juu sana.Endeleza kipaji chako pia tumia ubalozi wako kimataifa kuendeleza tamaduni yetu.Vilevile kuna wanamziki wengi wa changa wenye vipaji. Upatapo nafasi usiwe mbinafsi jaribu kuangalia jinsi gani ya kuwapa tafu ili nao watoke maana sanaa ni kurithishana hujui la kesho.Emmanuel-London
Zanzibar Car Hire Limited inakukaribisha Zanzibar ili uje ujifurahie na kuwatumbuiza Wazanzibari kwa miondoko yako ya kuvutia karibu Zanzibar 2010 hakika muziki wako unatugonga nyoyo zetu.
a,aleykum kaka,
naukubali sana mziki wako, najua wewe ni mwenyeji wa mkoa wa tanga, naomba utunge nyimbo ya kuusifia mkoa wa tanga kiutalii ili iweze kusaidia mkoa wa tanga kupata watalii wengi kutoka huko japan, kuna mapango ya amboni, vijiji vizuri kama sakura, kipumbwi. sina mengi kaka
Hongera mzee wa Buyuni.
Tatizo cd za nyimbo zako hazipatikani huku. bongoPia kama unaweza ebu zirudie zile za zamani na ukatoa cd ili tununue.kama zile masooud amekuwa jambazi
Hongera sana kaka kwa kazi zako nzuri- lakini zaidi huku tanga wapenzi wako wa muziki wanakuhitaji sana uwape raha. Tuwe pamoja kupitia Blog ya Tanga ambayo ni www.ankomo.blogspot.com (VIJIMAMBO VYA TANGA)
Hello Fresh Jumbe,
How are you today.
Your website and music is fabulous. I requested you to exchange the link. You have never comments.
Advise!
Richard Reward Kilonzo
www.world-tours-safaris.com
Kaka uko juu,nimepata kusikia kibao chako hiki cha Maisha ya Mjini kimetulia sana ndugu zako wa Tanga wanakulilia sana uje upige show walau Tanga Hotel,
Mie ni Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa Radio Mwambao Fm ya Tanga.
Oops!
Oops, you forgot something.